weekend movie star

movie and stories

Labels

Powered by Blogger.

Like Box

Blog Archive

Recent Movies

Angalia kipindi cha muvie star hapa.. leo tunae Queen Latifah



UDSM yafanya kumbukizi kwa wanafunzi waliofariki katika ajali ya basi la MAJINJA EXPRESS... wasome hapa

 Jumuiya ya chuo  kikuu cha Dar es salaam imefanya ibada maalum ya kumbukizi kwa wanafunzi wake watano waliofariki dunia katika ajali ya basi la majinja express iliyotokea mkoani iringa machi 11 mwaka huu na kusababisha vifo vya zaid ya watu 50.

Akizungumza katika ibada hiyo mkuu wa chuo cha fani za jamii profesa BELTRAM MAPUNDA amewataja wanafunzi hao kuwa ni ERICK KILEO,DAUD SOSTEN,JEREMIA WATSON na DIDIMO CHIWANGU wote wakiwa ni wanafunzi wa mwaka wa tatu katika fani ya shahada ya sanaa na elimu pamoja na FRANK MBAULE ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa pili katika fani ya shahada ya sanaa na elimu ambao walikuwa njiani kurudi chuoni mara baada ya kumalizika kwa likizo fupi.
 Aidha profesa MAPUNDA amesema kuwa ameupongeza uongozi wa chuo hicho kwa kwa kuona umuhimu wa kumbukizi hiyo ambayo imewapoteza vijana ambao walikuwa tegemeo kwa taifa huku akitoa wito kwa jumuiya ya chuo hicho kulifanyia utafiti suala la ajali za barabarani inayomaliza maisha ya watanzania walio wengi.

naibu makamu mkuu wa chuo YUNUS MGAYA 



Naye  naibu makamu mkuu wa chuo hicho prefesa YUNUS MGAYA amesema kuwa jumuiya ya chuo kikuu cha Dar es salaam imepata pengo kubwa kwa kuwapoteza wanafunzi watano kwa mkupuo katika ajali hiyo na kutoa pole kwa famuilia za marehemu hao huku akiwataka wanafunzi wa chuo hicho kuwa na utaratibu wa kuandika majina yao halisi pindi wawapo safarini kwani lolote linaweza kutokea.


Aidha kwa upande wake rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo  kikuu cha Dar es salaam GILBERT NELSON amesema wao kama wanafunzi wamesikitishwa na vifo vya wanafunzi wenzao na kusema kuwa jumuiya ya wanafunzi wa chuo hicho ilizipokea kwa mshtuko taarifa za vifo hivyo huku akitoa pole kwa wanafunzi wote wa chuo hicho
Raisi wa serikali ya wanafunzi DARUSO bw. GILBERT NELSON












SIBUKA_MAPINDUZI MAPYA KATIKA HABARI NA MATUKIO YA LIVE

kaa tayari mtanzania kwa mapindulizi ya habari za papo kwa hapo  pamoja na matukio muhimu ya kitaifa, midahalo, mahojiano na taarifa kubwa muhimu za kitaifa moja kwa moja kupitia SIBUKALIVE ya SIBUKA TV...
ni muda sasa wa kukupatia mtazamaji taarifa mbalimbali za kijamii, kisiasa na zote zinazohusu taifa letu moja kwa moja pindi zinapotokea kupitia teknolojia mpya na ya kisasa kabisa ya kurusha matangazo moja kwa moja (LIVE)...
HII pia ni fursa muhimu kwa mashirika maalumu yanayohusika na kuandaa na kuendesha midahalo na mazungumzo mbalimbali ya kitaifa kutumia chombo hiki kama njia ya haraka na uhakika kuwafikia hadhira husika kwa muda husika..
PIA hii ni nafasi kwa wale wote ambao wanatarajia kufanya matukio yakiwemo harusi, minada na mengine kama hayo na wangependa kurushwa live na SIBUKA TV iliyosambaa karibu tanzania nzima.
 
Copyright © 2015. SibukaWorld