Jumuiya ya chuo kikuu cha Dar es salaam imefanya ibada maalum ya kumbukizi kwa wanafunzi wake watano waliofariki dunia katika ajali ya basi la majinja express iliyotokea mkoani iringa machi 11 mwaka huu na kusababisha vifo vya zaid ya watu 50.

Akizungumza katika ibada hiyo mkuu wa chuo cha fani za jamii profesa BELTRAM MAPUNDA amewataja wanafunzi hao kuwa ni ERICK KILEO,DAUD SOSTEN,JEREMIA WATSON na DIDIMO CHIWANGU wote wakiwa ni wanafunzi wa mwaka wa tatu katika fani ya shahada ya sanaa na elimu pamoja na FRANK MBAULE ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa pili katika fani ya shahada ya sanaa na elimu ambao walikuwa njiani kurudi chuoni mara baada ya kumalizika kwa likizo fupi.
Aidha profesa MAPUNDA amesema kuwa ameupongeza uongozi wa chuo hicho kwa kwa kuona umuhimu wa kumbukizi hiyo ambayo imewapoteza vijana ambao walikuwa tegemeo kwa taifa huku akitoa wito kwa jumuiya ya chuo hicho kulifanyia utafiti suala la ajali za barabarani inayomaliza maisha ya watanzania walio wengi.

Aidha kwa upande wake rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam GILBERT NELSON amesema wao kama wanafunzi wamesikitishwa na vifo vya wanafunzi wenzao na kusema kuwa jumuiya ya wanafunzi wa chuo hicho ilizipokea kwa mshtuko taarifa za vifo hivyo huku akitoa pole kwa wanafunzi wote wa chuo hicho
Akizungumza katika ibada hiyo mkuu wa chuo cha fani za jamii profesa BELTRAM MAPUNDA amewataja wanafunzi hao kuwa ni ERICK KILEO,DAUD SOSTEN,JEREMIA WATSON na DIDIMO CHIWANGU wote wakiwa ni wanafunzi wa mwaka wa tatu katika fani ya shahada ya sanaa na elimu pamoja na FRANK MBAULE ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa pili katika fani ya shahada ya sanaa na elimu ambao walikuwa njiani kurudi chuoni mara baada ya kumalizika kwa likizo fupi.
| naibu makamu mkuu wa chuo YUNUS MGAYA |
Naye naibu makamu mkuu wa chuo hicho prefesa YUNUS MGAYA amesema kuwa jumuiya ya chuo kikuu cha Dar es salaam imepata pengo kubwa kwa kuwapoteza wanafunzi watano kwa mkupuo katika ajali hiyo na kutoa pole kwa famuilia za marehemu hao huku akiwataka wanafunzi wa chuo hicho kuwa na utaratibu wa kuandika majina yao halisi pindi wawapo safarini kwani lolote linaweza kutokea.
Aidha kwa upande wake rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam GILBERT NELSON amesema wao kama wanafunzi wamesikitishwa na vifo vya wanafunzi wenzao na kusema kuwa jumuiya ya wanafunzi wa chuo hicho ilizipokea kwa mshtuko taarifa za vifo hivyo huku akitoa pole kwa wanafunzi wote wa chuo hicho
| Raisi wa serikali ya wanafunzi DARUSO bw. GILBERT NELSON |
0 comments:
Post a Comment